Hospitali ya Survival ipo mbioni kupanua uwezo wa kutoa huduma zake. Sasa kuanzia mwezi wa June 2025, hospitali hiyo itakuwa kituo bora cha upasuaji. Amesema hayo Mkurugenzi mkuu wa Hospitali hiyo CPA. S.K.Rutenge, wakati akitoa ufafanuzi juu ya huduma zinazo tolewa na zile ambazo wanatarajia kuanza kuzitoa. Ameongeza kuwa kwa sasa huduma za OPD, RCH, Kinywa na Meno, Macho, na Mionzi ya Utrasound, Kujifungua kwa akina Mama, kulazwa kwa Wagonjwa, Ambulance na nyingine nyingi Hutolewa kila siku. Hata hivyo baadhi ya huduma hutolewa kwa kushirikiana na Madaktari Bingwa kutoka hospitali za rufaa.