UTANGULIZI
Hospitali ya Survival ni hospitali binafsi iliyosajiliwa rasmi kwa ngazi ya Wilaya kwa mujibu wa masharti ya Sheria ya Hospitali Binafsi (Kanuni) Sura ya 151, kwa namba ya usajili 12151. Iko Rushe, Mabira, katika Wilaya ya Kyerwa, Mkoa wa Kagera.
Hospitali hii imezindua idara zote kuu za utoaji huduma ambazo ni pamoja na Dawa (Pharmacy), Maabara, Uzazi, Upasuaji (Theatre), Huduma ya Afya ya Mama na Mtoto (RCH), Wodi ya Wajawazito, Wanaume, Mionzi (Radiology), Huduma ya Dharura, Huduma kwa Watoto Wachanga (Neonatal), Chumba cha Kuhifadhia Maiti (Mortuary), na Wodi za Wagonjwa wa Kulazwa.
Hospitali ya Survival ni kituo kipya kilichoanzishwa na kumilikiwa na kampuni ya NSG CO. LTD yenye makao makuu katika mkoa wa Geita. Hospitali inatoa mazingira bora ya kufanyia kazi na ina miundombinu yote mihimu na mizuri.
Hospitali kwa sasa inatafuta wafanyakazi walio na ari ya kazi na wanaopenda kuhudumia wagonjwa katika fani zifuatazo:
Fungua JOB OPPORTUNITIES-SURVIVAL HOSPITAL,AUGUST 2025 (1) kupata tangazo la AJIRA.
“Hospitali ya Survival ni Sehemu ya Tumaini Jema”
NYOTE MNAKARIBISHWA