LOGO YA SURVIVAL
Logo hii ilibuniwa na Mr. Rutenge au Dr. Survival na kupewa namba ya usajili wa alama za Biashara (Logo) TZ/S/2023/1096 na BRELA mnamo 2023.
Sasa zitambue alama muhimu katika logo hiyo.
ALAMA ZINAZO ONEKANA
- MIKONO MIWILI
- SKAFU YA BLUE
- ALAMA YA MOYO
ALAMA ZA KUFIKIRIKA
- Alama ya Upendo na Huruma
- Muingiliano wa upendo na ushirikiano wa kibinadamu
- Alama ya Amani,utulivu na Ulinzi wa Asili
- Usalama, Maadili na Utulivu wa Mpokeaji
- Nguvu ya asili na moyo wa kujitoa
- Nguvu ya kusadia ukiwa kwenye sehemu salama.
MAANA YA ALAMA HIZO
Mkono wa Chini
Ni mkono wa kuomba msaada. Ukiwakilisha jamii. Jamii tunazo tokea siku zote huitaji msaada wetu kuweza kuendelea
Mkono wa Juu
Mkono unaotaka kutoa msaada. Huyu ni mtu kutokea katika jamii inayoomba msaada na hivyo anataka kurudisha msaada katika jamii yake na ndiyo maana mkono unao omba na ule unao taka kutoa zina fanana.
Mikono kuwa na Rangi sawa
Mtoa msaada na wapokea msaada wote hutokea jamii moja. Hivyo wote wana asili moja.
Mikono kutogusana
Mbali na moyo wa kusaidia jamii hata siku moja huwezi kutosheleza wote, kuna kundi litakupinga. Hivyo ni muhimu kusaidia bila kugusana.
SKAFU YA BLUE
Hii inawakilisha amani, utulivu na ulinzi wa asili. Uwepo wa hii kwenye logo inawakilisha uimarishwaji wa ulinzi juu ya changamoto tuzipitiazo katika jamii zetu.
ALAMA YA MOYO
Hii imesimama au imewekwa kuonesha upendo, tulionao kwenye jamii yetu.
Moyo kuwa na rangi nyekundu
Rangi yekundu iliyo zunguka moyo ni ishara ya kujitoa kwa ajili ya jamii.
Rangi nyeupe kwenye hiyo logo
Rangi hii imezunguka mikono ya muomba msaada na mpokea msaada. Hii inaonesha umuhimu wa kusaidia ukiwa huru kufanya hivyo.