Hospital ya Survival iliopo Kyerwa Mkoani Kagera sasa kutoa elimu ya umuhimu wa kutumia huduma za afya badala ya kuwaficha wagonjwa nyumbani na kuwanunulia dawa au jamii kununua dawa na kutumia bila kupata ushauri wa Daktari. Suala hili limekuwa likiongezeka katika jamii zetu ambapo watu huenda katika maduka maduka ya dawa na kununua dawa kisha kutumia kabla ya kupima. Kauli mbiu yetu ya “Tibu ugonjwa usitibu dalili” inategemewa kutumika kuhamasisha jamii kutumia huduma za afya ili kupata matibabu sahihi.