Survival hospitalSurvival hospitalSurvival hospital
Geita - Tanzania
+255 767 710 320

TIBU UGONJWA USITIBU DALILI

Katika mwendelezo wa kuendelea kuongeza uelewa wa umuhimu wa huduma za afya katika Jamii. Hospitali ya Survival iliyopo Mabira Wilayani Kyerwa, inatarajia kuzindua kampaini yake ya TIBU UGONJWA USITIBU DALILI, makusudi ya kampani hii ni kufikisha ujumbe wa umuhimu wa kutumia vituo vitowavyo huduma za afya kupima afya zao kabla ya kutumia dawa.

Imekuwa kawaida kwa jamii zetu kwenda katika maduka ya dawa na kununua dawa kisha kutumia bila ya kuwa na ushauri wa Daktari pia bila ya kupima. Hii huifanya jamii kuamini wanaumwa hata kama dalili hızo zinatokana na uchovu. Au ilipaswa kuwa suala ya kunywa maji na kupumzika. #Tibuugonjwausitibudaili