Survival hospitalSurvival hospitalSurvival hospital
Geita - Tanzania
+255 767 710 320

KUITWA KUSAINI MIKATABA YA AJIRA NA KURIPOTI KAZINI

Uongozi wa Survival Hospital unapenda kuwashukuru wote mlio onesha nia ya kutaka kufanya kazi na sisi. Tunapenda kuwashukuru asanteni sana. Pia tunashukuru kwa mapendekezo yenu. Tuna imani tumeyafanyia kazi.

Tunapenda kuchukua nafasi hii kuwambia kuwa usahili umekamilika na tayari tumechagua timu ya  kuanza nao. Tunaimani kuwa timu yetu ya usahili imeweza kuwapigia simu wote na kujadiliana juu ya mishahara ya kuanza nayo. Tunawahaidi kuwa kile mlichokubalina  kitatekelezwa na kitaendelea kuboreshwa kadili ya mazingira yatakavyo jitokeza baada ya kufungua hospitali yetu.

Hivyo,  kwa wote walio chaguliwa mtatumiwa email pamoja na kupigiwa simu kufahamishwa siku ya kuja kusaini mikataba na siku ya kuripoti kazini.  Kwa wale ambao hawajachaguliwa bado tunania ya kufanya kazi ninyi   na tutawataarifu pale tutakapo kuwa na uhitaji.

TUNAWASHUKURU SANA

SUVIVAL HOSPITAL 

”SISI NI SEHEMU YA TUMAINI JEMA”